Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Mawaziri wa fedha kutoka nchi za G20 waikashifu Marekani

media Rais wa Argentina Mauricio Macri akizungumza wakati wa mkutano wa mawaziri wa fedha kutoka nchi za G20. 20 Machi 2018. Argentine Presidency/Handout via REUTERS

Nchi ya Marekani imesema haitaki vita ya kibiashara kutokana na tangazo lake kuhusu kodi mpya za forodha lakini ikasisitiza kuwa haitamuogopa mtu, haya ni matamshi ya waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin baada ya mkutano wake na mawaziri wa fedha kutoka nchi za G20.

Vita ya kibiashara sio lengo letu lakini hatuiogopi alisema Mnuchin wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa fedha kutoka nchi za G20 waliokutana mjini Buenos Aires Argentina.

Matamshi ya Mnuchin anayatoa wakati huu nchi yake ikikosolewa kutokana na kutangaza kutoza ushuru wa forodha kwa bidhaa za Chuma na Aluminium zinazotoka nje ya Marekani.

"lazima tujiandae kuchukua hatua kwa manufaa ya Marekani katika kulinda uhuru na usawa wa biashara. katika kufanya hivi mara zote kuna hatari," alisema Mnuchin.

Mnuchini alikuwa akizungumza baada ya mawaziri hao wa fedha kukubaliana kulaani hatua ya Marekani.

Taarifa ya pamoja ya mawaziri hawa imetolewa ikiwa ni siku moja tu imebaki kabla ya kuanza kutumika rasmi kwa sheria iliyotiwa saini na rais Trump kuhuus ushuru wa forodha kwa bidhaa za nje.

Mawaziri hao wamesema kuwa hatua ya Marekani haina lengo jema katika ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi wanachama, na kwamba kodi iliyotangazwa kutozwa na Marekani itaathiri biashara baina ya mataifa yao.

Wakati akitia saini mkataba huo rais Trump alisema lengo sio kuzikomoa nchi zinazofanya biashara na Marekani lakini imelenga katika kuimarisha viwanda vyake vya ndani na kuzuia bidhaa zisizo na ubora kuingia nchini Marekani.

Nchi ya Canada na China zimekuwa nchi za awali kukashifu hatua ya Marekani kwa kuwa zimekuwa zikifanya biashara kubwa ya Chuma na Aluminium kwa taifa la Marekani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana