Pata taarifa kuu
UINGEREZA-URUSI-JASUSI

Uingereza na washirika wake wasisitiza Urusi ilimpa sumu jasusi wake wa zamani

Nchi ya Uingereza na washirika wake wameulaumu moja kwa moja utawala wa Moscow kwa kuhusika na matumizi ya sumu dhidi ya jasusi wake wa zamani, hatua iliyosababisha mzozo wa kidiplomasia wakati huu Marekani ikitangaza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi kwa kujaribu kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016. 

Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza  Boris Johnson
Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson REUTERS/Simon Dawson
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Marekani wamesema kuwa hakuna maelezo mengine ya ziada kuwa Urusi haikuhusika na tukio la kwenye mji wa Salisbury dhidi ya jasusi huyo wa zamani Sergei Skripal na binti yake Yulia ambapo ilitumia sumu aina ya Novichok inayoathiri mishipa ya fahamu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema nchi yake iko pamoja na Uingereza na inakashifu kitendo kilichofanywa na utawala wa Urusi.

Rais Macron amesema kitendo cha Urusi hakikubaliki na kinastahili kulaaniwa.

“Nitatangaza hatua za kuchukua katika siku zijazo,” alisema rais Macron.

Kiongozi huyo wa Ufaransa atajadili suala hili na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye atazuru jijini Paris siku ya Ijumaa.

Mataifa ya Marekani, Ujerumani na Ufaransa yamesema kushambuliwa kwa Uingereza ni kushambuliwa kwao wote.

Urusi imekanusha madai ya kumpa sumu jasusi huyo wa zamani na kuongeza kuwa, hivi karibuni italipiza kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia wa Uingereza kutoka nchini humo.

Uingereza wiki hii iliwafukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi na kuwaambia waondoke nchini humo ndani ya wiki moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.