Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAHAKAMA

Mahakama nchini Ufaransa yaamua gaidi hatari aendelee kutumikia kifungo cha maisha

Ilich Ramírez Sánchez anayefahamika kwa jina maarufu la Carlos the Jackal, amepoteza rufaa ya kupinga hukumu ya maisha jela baada ya kupatikana na kosa la kutekeleza matukio ya kigaidi jijini Paris miaka 44 iliyopita.

Mchoro wa Ilich Ramirez Sanchez maarufu kama Carlos the Jackal.
Mchoro wa Ilich Ramirez Sanchez maarufu kama Carlos the Jackal. Benoit PEYRUCQ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Majaji wamesema ushahidi unaonesha kuwa Sanchez mwenye umri wa miaka 68,  ndiye aliyehusika na matukio ya kigaidi na hata kushuka guruneti.

Raia huyo wa Venezuela ni gaidi ambaye alikamatwa mwaka 1994 nchini Sudan na kusafirishwa jijini Paris nchini Ufaransa ili kufunguliwa mashtaka.

Alipatakana na makosa 16 ya mauaji ambayo ni pamoja na kusababisha kifo cha jasusi wa serikali ya Ufaransa na maafisa wawili wa inteljensia.

Akiwa gerezani, Sanchez alifunguliwa mashtaka ya kupanga shambulizi la kigaidi lililosababisha vifo vya watu 11 na kuwajeruhi wengine 150.

Mwaka 2011 na 2017, gaidi huyo alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kutekeleza mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.