Pata taarifa kuu
UINGEREZA-URUSI-JASUSI

Uingereza yawafukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi baada ya jasusi kupewa sumu

Uingereza imesema itawafukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi baada ya Moscow kukataa kufafanua namna jasusi wake Sergei Skripal alivyopewa sumu mjini Salisbury wiki iliyopita.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akitangaza hatua dhidi ya Urusi akiwa bungeni Machi 14 2018
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akitangaza hatua dhidi ya Urusi akiwa bungeni Machi 14 2018 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Theresa May amesema wanadiplomasia hao wana wiki moja kuondoka nchini Uingereza.

Aidha, amefuta mwaliko aliokuwa ametoa kwa Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov lakini pia Familia ya Malkia haitahudhuria fainali ya kombe la dunia mwezi Juni.

Hatua hii imekuja baada ya uchunguzi wa Uingereza kubaini kuwa serikali ya Urusi ilihusika katika tukio la kumpa sumu Skripal na binti yake Yulia kwa lengo la kumuua.

Skripal na binti yake wanaendelea kupata matibabu jijini London baada ya tukio hilo. Raia huyo wa Urusi, alikuwa Jasusi wa Uingereza katika nchi yake kwa muda mrefu.

Nick Bailey afisa wa Polisi ambaye alikwenda kumsaidia Jasusi huyo wa zamani pia aliathiriwa na sumu hiyo na amelazwa pia hospitalini.

Urusi imeendelea kusisitiza kuwa, haikuhusika kwa vyovyote vile katika jaribio la kumuua jasusi huyo.

Ubalozi wa Urusi jijini London umelaani hatua hiyo ya serikali ya Uingereza na kusema haikubaliki.

Wakati uo huo, Uingereza imetishia kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili suala hili.

Wakati uo huo, Uingereza imewataka raia wake kuwa makini wanapokwenda Urusi kwa kile inachosema huenda wakasumbuliwa kwa sababu ya uamuzi uliochukuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.