Pata taarifa kuu
UJERUMANI-MERKEL-SIASA

Kansela Merkel achaguliwa na kuapishwa kwa muhula wa nne

Angela Merkel ameapishwa kuwa Kansela wa Ujerumani kwa muhula wa nne wa miaka minne, baada ya wabunge kumchagua tena siku ya Jumatano kuendelea kuongoza taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Ulaya.

Angela Merkel akiwa na rais Frank-Walter Steinmeier, baada ya kuapishwa kwa muhula wa nne kama Kansela wa Ujerumani Machi 14 2018
Angela Merkel akiwa na rais Frank-Walter Steinmeier, baada ya kuapishwa kwa muhula wa nne kama Kansela wa Ujerumani Machi 14 2018 REUTERS/Fabrizio Bensch
Matangazo ya kibiashara

Wabunge 364 walipiga kura za kumchagua Kansela Merkel huku 315 wakipinga na tisa kuamua kutoshiriki katika zoezi hilo la kihistoria.

Hatua hii imekuja baada ya Merkel kufanikiwa kuunda serikali ya muungano hivi karibuni baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka uliopita na chama chake cha CDU kushindwa kuunda serikali peke yake kwa sababu ya idadi ndogo ya wabunge.

Bi. Merkel ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo ya Ujerumani tangu mwaka 2005 na kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hiyo ya juu nchini humo, huenda huu nido ukawa muhula wake wa mwisho katika nafasi hiyo licha ya kutokuwepo kwa ukomo wa mihula.

Kazi kubwa inayomsubiri ni namna ya kuendelea kuimarisha uchumi wa taifa lake, kuhimiza Umoja wa Ulaya pamoja na kushughulikia suala la wakimbizi wanaoiendelea kuingia barani Ulaya hasa wale wanaokimbilia nchini Ujerumani.

Siku ya Ijumaa wiki hii, Kansela Merkel anatarajiwa kwenda jijini Paris kukutana na rais Emmanuel Macron kujadili mabadiliko ndani ya Umoja wa Ulaya kuelekea Mkutano mkuu wa wakuu wa nchi kati ya tarehe 22-23 mwezi huu wa Machi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.