May: Urusi ilimpa sumu jasusi wetu Sergei Skripal
Nchi washirika wa Uingereza, zimetangaza kuiunga mkono nchi hiyo baada ya Waziri Mkuu Theresa May kudai kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa utawala wa Moscow ulihusika katika kutumia kemikali zinazoathiri mishipa ya fahamu kwa jasusi wake wa zamani wa Urusi.
Imechapishwa:
Katika matamshi yake ya kwanza kwa umma Waziri Mkuu May amesema wana uhakika kuwa uchunguzi wao na tathmini iliyofanywa na idara za usalama umeonesha uwezekano kuwa Urusi ilihusika katika jaribio la kumuua Sergei Skripal na binti yake Yulia.
"Ni wazi kuwa walipewa sumu kwa mpango wa serikali ya Urusi,"
"Serikali baada ya Uchaguzi, imebaini kuwa Urusi ilihusika na kungependa tusikie kutoka kwao iwapo wana pingamizi yoyote," alisema Waziri Mkuu May.
Wawili hao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali moja jijini London.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema wanakubaliana na Uingereza na kuongeza kuwa wahusika wachukuliwe hatua kali.
Hata hivyo, Urusi imeendelea kukanusha madai ya kuhusika katika jaribio la kutaka kumuua jasusi hiyo ambaye amepewa uraia nchini Uingereza.