Pata taarifa kuu
UINGEREZA-URUSI-JASUSI

May: Urusi ilimpa sumu jasusi wetu Sergei Skripal

Nchi washirika wa Uingereza, zimetangaza kuiunga mkono nchi hiyo baada ya Waziri Mkuu Theresa May kudai kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa utawala wa Moscow ulihusika katika kutumia kemikali zinazoathiri mishipa ya fahamu kwa jasusi wake wa  zamani wa Urusi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May REUTERS/Simon Dawson
Matangazo ya kibiashara

Katika matamshi yake ya kwanza kwa umma Waziri Mkuu May amesema wana uhakika kuwa uchunguzi wao na tathmini iliyofanywa na idara za usalama umeonesha uwezekano kuwa Urusi ilihusika katika jaribio la kumuua Sergei Skripal na binti yake Yulia.

"Ni wazi kuwa walipewa sumu kwa mpango wa serikali ya Urusi,"

"Serikali baada ya Uchaguzi, imebaini kuwa Urusi ilihusika na kungependa tusikie kutoka kwao iwapo wana pingamizi yoyote," alisema Waziri Mkuu May.

Wawili hao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali moja jijini London.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema wanakubaliana na Uingereza na kuongeza kuwa wahusika wachukuliwe hatua kali.

Hata hivyo, Urusi imeendelea kukanusha madai ya kuhusika katika jaribio la kutaka kumuua jasusi hiyo ambaye amepewa uraia nchini Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.