Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Taasisi kuu Uingereza kuchunguza rasimu ya sheria ya kujitoa EU

media Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May wakati wa hotuba yake kuhusu kujitoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Florence, Septemba 22, 2017. REUTERS/Maurizio Degl'Innocenti

Taasisi kuu nchini Uingereza imeanza mchakato wa kuchunguza muswada wa sheria wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya, rasimu ya shria muhimu ambayoitapelekea kuibuka kwa mijadala mikali.

Taasisi hiyo imetoa wito kwa serikali kupitia upya nakala yake.

Muswada huo ulipitishwa na wajumbe wa Baraza la bunge mnamo Januari 17, baada ya hali ya sintofahamu kuibuka nchini humo nchi hiyo kutangaza kuanzisha mchakato wa kujitoa katia Umoja wa Ulaya.

Muswada huu wa sheria utaruhusu Uingereza kuendelea shughuli zake wakati imejitenga na Umoja wa Ulaya Machi 29, 2019. Sheria hiyo itasitisha mamlaka ya sheria ya Ulaya kwenye sheria za kitaifa za Uingereza na kuingiza ndani ya sheria za Uingereza sheria zinazohusu jamii mbalimbali nchini humo.

Katika ripoti iliyotolewa siku ya Jumatatu, Kamati ya Kikatiba ya Mahakama Kuu iliagiza serikali ya Theresa May kufanya mageuzi makubwa, ikisema kuwa "muswada wa sheria, kama ulivyoandikwa, una kasoro nyingi".

Kamati hiyo inashutumu utaratibu uliyopendekezwa na serikali "kuiga" baadhi ya sheria za Ulaya, ambazo kwa mtazamo wake zitasababisha "kutokuwa na uhakika na utata wa kisheria".

Wajumbe wa kamati hiyo pia wana wasiwasi juu ya mamlaka makubwa ambayo muswada huo unaipa serikali katika masuala ya sheria, wakisema kuwa "unawapa mamlaka makubwa mawaziri kuliko ilivyokubaliwa kikatiba".

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana