Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-USHIRIKIANO

Emmanuel Macon kuendelea na mageuzi alioanzisha

Raia wa Ufaransa wamesherehekea kwa furaha Mwaka Mpya 2018, huku rais Emmanuel Macron, katika hotuba yake iliyodumu dakika zisizozidi 20, akitangaza kuendelea na mageuzi yaliyoanzishwa nchini Ufaransa na kutoa maoni yake ya ahadi ya Ufaransa kwa ulimwengu. Pia alikumbusha nia yake kwa ujenzi wa Ulaya.

Hotuba ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yarushwa moja kwa moja kweye televisheni., Desemba 31, 2017.
Hotuba ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yarushwa moja kwa moja kweye televisheni., Desemba 31, 2017. REUTERS/John Schults
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa aliwatakia raia wa Ufaransa, jeshi , vikosi vya usalama na wauguzi Heri ya Mwaka Mpya 2018, akiwataka kuzingatia kazi kwa maslahi ya taifa.

Rais Macron alisema ataendelea kutekeleza kilichompelekea achaguliwe kuwa rais wa Ufaransa.

"Nitaendelea kufanya yale yalio nipelekea nachaguliwa kama rais wa Ufaransa." Emmanuel Macron amewahakikishia raia wa Ufaransa kwamba mwaka 2018 "utakuwa" ni wenye miradi kwa maeneo ya vijijini, kupatikana kwa mfumo wa kidijitali katika maeneo yenye makazi, bila kusahau wakulima, ambao wanatakiwa "kuishi vizuri, bila bughdha".

Rais wa Ufaransa amesema Ufaransa "nchi yenye nguvu", mwaka 2018 itakuwa na "mahitaji ya ulimwengu wote" na "kujitolea kwa masuala ya kibinadamu". Rais MAcron amesema Ulaya na ulimwengu kwa ujumla lazima usimame na kupambana dhidi ya "ugaidi unaoendeshwa na wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali" na dhamira yake ni "kushinda vita hivi". Lakini pia kusimamia amani hali na mali, kushirikiana ili "kuhakikisha utulivu katika nchi mbalimbali duniani".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.