Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Maelfu ya raia waingia mitaani kuunga mkono uhuru wa Catalonia Brussels

media Maelfu ya watu wamiminika mitaani Brussel kuunga mkono uhuru wa Catalonia. /REUTERS/Yves Herman

Zaidi ya watu 50,000 wameandamana leo Alhamisi mjini Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji kuunga mkono uhuru wa Catalonia na rais wa zamani wa eneo hilo Carles Puigdemont, ambaye alikimbilia mjini humo kwa kuhofia kukamatwa na serikali kuu ya Uhispania.

Polisi ya Ubelgiji imebaini kwamba waandamanaji 45,000 walikusanyika katika wilaya moja ya Brussels kabla ya kiongozi wao kuhutubia umati wa watu.

Miongoni mwa waandamanaji, wengi wao walikuja wakitokea Catalonia, baadhi walikua wakibebelea mabango ambapo wanashtumu Umoja wa Ulaya kutumiwa na Madrid katika mgogoro huo.

"Brussels ni kipaza sauti ili kila mmoja ajue kwamba hatuna demokrasia kamili nchini Uhspania na kwamba Catalonia imekuwa kila mara na matatizo na Uhispania," amesema Gloria Cot, alieshiriki maandamano hayo akitokea Barcelona.

Makamu wa rais wa Tume ya Ulaya Frans Timmermans alikaribisha jinsi maandamano yalivyofanyika katika "mazingira mazuri" lakini ameonya kuwa Umoja wa Ulaya hauwezi kubadilisha mtazamo wake kana kwamba mgogoro kati ya Barcelona na Madrid ni suala la ndani ambalo Umoja wa Ulaya haupaswi kuingilia kati.

Serikali ya Uhispania ilifuta mamlaka ya Catalonia baada ya kutangazwa uhuru wa eneo hilo. Tangazo lililotolewa na Carles Puigdemont.

Uchaguzi katika eneo la Catalonia umepangwa kufanyika Desemba 23, ambapo viongozi wa waliotimuliwa, ikiwa ni pamoja na Carles Puigdemont, watawania.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana