Pata taarifa kuu
UHISPANIA-CARLES-HAKI-SIASA

Puigdemont atarajia kubaki Ubelgiji

Rais wa zamani wa Catalonia, nchini Uhispania Carles Puigdemont ametangaza leo Jumatano nia yake ya kubaki "kwa sasa" nchini Ubelgiji, siku moja baada ya Uhispania kuondoa waranti wa kimataifa uliyotolewa dhidi yake.

Aliekua rais wa Catalonia Carles Puigdemont ametangaza nia yake ya kubaki Ubelgiji.
Aliekua rais wa Catalonia Carles Puigdemont ametangaza nia yake ya kubaki Ubelgiji. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Je! Naweza kutembea bila matatizo katika Umoja wa Ulaya? Kwa sasa sina jibu (...) Nitakaa hapa," Bw Puigdemont amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Brussels, nchini Ubelgiji.

Carles Puidgemont alikuwa akiongozana na wasaidizi wake wanne waliomfuata Brussels baada ya kutangazwa kwa uhuru wa Catalonia Oktoba 27 na kufutwa kwa mamlaka ya eneo hilo kwa jitihada za Madrid.

Mahakama Kuu ya Uhispania ilitangaza siku ya Jumanne kufutwa kwa waranti wa kimataifa wa kukamatwa dhidi ya viongozi watano wa Catalania, ikieleza kuwa walionyesha nia yao ya kurudi nchini Uhispania kushiriki katika uchaguzi wa Catalania tarehe 21 Desemba, lakini bado wanatafutwa kwa uasi, uchochezi na uharibifu wa fedha za umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.