Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Makamu wa rais wa zamani wa Catalonia kuendelea kuzuiliwa

media Aliekua makamu wa rais wa Catalonia Oriol Junqueras (katikati) na mwenzake wa chama cha "Junts pel Si" Marta Rovira (kushoto), washirika wa uchaguzi wa kikanda wa Desemba 21. Hapa, ilikua Oktoba 14, 2017 Barcelona. PAU BARRENA / AFP

Mahakama Kuu ya Uhispania, leo Jumatatu imekataa kumuachia kwa dhamana aliyekuwa makamu wa rais Catalania Oriol Junqueras, pamoja na waziri wa zamani Joaquim Forn na viongozi wa mashirika mawili yanayotetea uhuru wa Catalonia, ANC na Omnium Cultural.

Viongozi wa mashirika hayo Jordi Sanchez na Jordi Cuixart, wanashutumiwa uasi na uchochezi.

Mawaziri wa zamani wengine sita, waliowekwa kizuizini kwa kusubiri uchunguzi ukamilike kuhusu tangazo la uhuru wa eneo hilo waliachiwa kwa dhamana ya euro 100,000.

Tangazo la uhuru lililotolewa na serikali ya Catalonia Oktoba 27 limesababisha serikali kuu ya Uhispania kutwaa mamlaka yote ya eneo hilo na imeitisha kura ya mapema tarehe 21 Desemba.

Wajumbe nane wa zamani wa serikali ya Catalonia walilikwa kizuizini Novemba 2 kwa kosa la uasi na ubadhirifu. Wanaomba kuachiliwa kwa dhamana ili waweze kushiriki katika kampeni hiyo.

Rais wa zamani wa Catalania Carles Puigdemont na wanachama wanne wa baraza la mawaziri walikimbilia Ubelgiji. Waranti za kukamatwa dhidi yao na mahakama ya Ubelgiji wamewachia huru kwa dhamana.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana