Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Viongozi wa Ulaya kukutana kwa kufufua mchakato wa kuindoa Uingereza katika EU

Viongozi Ishirini nane wanatazamiwa kukutana Alhamisi Oktoba hii 19 mjini Brussels, nchini Ubegiji, kwa Baraza la Ulaya. Kando ya mkutano Emmanuel Macron atakutana na kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel na wa Uhispania, Mariano Rajoy.

David Davis, Waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya kuiondoa nchi katika Umoja wa Ulaya (kushoto) na Michel Barnier, mkuu wa mazungumzo ya kutoka Umoja wa Ulaya kuhusu kujiondoa kwa Uindereza katika EU, Brussels, Septemba 25, 2017.
David Davis, Waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya kuiondoa nchi katika Umoja wa Ulaya (kushoto) na Michel Barnier, mkuu wa mazungumzo ya kutoka Umoja wa Ulaya kuhusu kujiondoa kwa Uindereza katika EU, Brussels, Septemba 25, 2017. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Sehemu kubwa ya mkutano huu itagubika mchakato wa kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, ambapo mazungumzo yanatakiwa kuongeza kasi ya kufikia tarehe ya mwisho ya miaka miwili, ikiwa ni pamoja na kuridhiwa kwa bunge, kulingana na Ibara maarufu ya 50 ya Mkataba wa Lisbon.

Hadi mapema mwezi huu, mazungumzo yalikua bado hayajaza matunda yoyote, kwa sababu kulingana na mtazamo wa London, ingekuwa ni pigo kubwa kwa Theresa May kutoa hisia za aina yoyote kwa kukubali chochote kabla ya kongamano ya chama chake, chama cha Conservative. Kwa kifupi, vikao vinne vya mazungumzo havijazaa matunda yoyote.

Kikao cha tano hakikuanzisha mazungumzo yoyote. Kwa hiyo, Washirika ishirini na saba wa Theresa May, waliokutana tarehe19 na 20 Oktoba, hawajaweza kuona maendeleo yoyote katika mazungumzo ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya ambayo, kulingana na mchakato ambao Uingereza ilitumia, mazungumzo hayo yangeliruhusu kufunguliwa sambamba mazungumzo menginekuhusu mahusiano ya baadaye ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Pamoja na majaribio ya Uingereza ya kufutilia mbali mazungumxzo hayo kati ya nchi hizo ishirini na saba na Msimamizi mkuu wa mazungumzo hayo wa Umoja wa Ulaya, Michel Barnier, kwa sasa ni vigumu mazungumzo kama hayo kufanyika. Kwa upande mwingine, Umoja wa Ulaya utakua na mengi ya kuzungumza kuhusu Uingereza, ambapo itatakiwa kuwa na maendeleo ya kutosha kabla ya mwisho wa mwezi Desemba ili hatimaye kuzungumzia hatma ya Umoja wa Ulaya baada ya Uingereza kujiondoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.