Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Serikali ya Uhispania yakutana kwa dharura

Siku moja baada ya hotuba ya Carles Puigdemont kutangaza kusitisha mchakato wa uhuru katika jimbo lake, serikali kuu ya Uhispania inakutana ili kujadili hali inayoendelea katika jimbo hilo.

Rais wa Catalonia Carles Puigdemont akisaini hati ya kujitenga, Barcelona tarehe 10 Oktoba 2017.
Rais wa Catalonia Carles Puigdemont akisaini hati ya kujitenga, Barcelona tarehe 10 Oktoba 2017. REUTERS/Albert
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo wa dharura unafanyika Jumatano hii, wakati ambapo rais wa Catalonia alisaini hati ya kujitenga kwa jimbo la Catalonia, licha ya kusita kutangaza uhuru wa jimbo hilo, akisema kuna haja ya kufanya mazungumzo katika ngazi ya kitaifa na ile ya kimataifa kuhusu uhuru a Catalonia.

Kikao cha Baraza la Mawaziri, chini ya uenyekiti wa Mariano Rajoy, Waziri Mkuuu wa Uhispania kimepangwa kufanyika saa 9 asubuhi saa za Uhispania, kuamua hatua za kuchukua siku moja baada ya kikao cha ubunge cha bunge Catalonia.

Kutokana na shinikizo kutoka pande zote, pamoja na Ulaya, rais wa jimbo la Catalonia, Carles Puigdemont, aliahidi kubadilisha Catalonia kuwa "Jamhuri" huru, huku akiomba kusitishwa kwa mchakato huo kwa kusubiri kupata "ufumbuzi" kutoka katika mazungumzo na serikali kuu ya Madrid.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.