Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Carles Puigdemont asaini hati ya kujitenga kwa jimbo la Catalonia

media Rais jimbo la Catalonia Carles Puigdemont mbele ya Bunge la Catalonia tarehe 10 Oktoba 2017. REUTERS/Albert Gea

Kiongozi wa jimbo la Catalonia nchini Uhispania, Carles Puigdemont, ameahidi uhuru wa jimbo hilo lakini amejiuia kutangaza uhuru wake akibaini kwamba mchakato huo huenda ukaligawa jimbo la Catalonia.

Carles Pugdemont, amesaini hati ya kuwa huru, lakini ametoa muda zaidi wa mazungumzo na serikali kuu ya Uhispania kuhusiana na kujitenga jimbo la Catalonia.

Akiwa mbele ya bunge la Catalonia mjini Barcelona, licha ya kuchelewesha hotuba yake kwa muda wa saa moja, Bw. Puigdemont alizungumzia kuhusu "madhara ya kisiasa" ya kura ya maoni ykuhusu uhuru wa jimbo la Catalonia, akisisitiza haja ya "kupunguza mvutano" na serikali kuu ya Madrid. Kwa mujibu wa Carles Puigdemont, Catalonia imepata haki ya kuwa taifa huru.

Carles Puigdemont aliomba Bunge kusitisha utekelezaji wa mchakato wa uhuru ili kuweza kuzungumza na serikali kuu ya Madrid. Wakati huo huo Madrid imefutilia mbali mazungumzo ya aina yoyote na viongozi wa Catalonia.

Carles Puigdemont, mwandishi wa habari wa zamani mwenye umri wa miaka 54, amesita kutangaza uhuru wa Cataloni, licha ya kufafanua hoja yake baada kura ya maoni ya kujitawala kwa jimbo la Catalonia, kura ambayo ilipigwa marufuku Oktoba 1, ambapo serikali yake imehakikisha kwamba kura ya "Ndiyo" ilishinda kwa zaidi ya 90% kwa kiwango cha ushiriki wa 43%.

"Nahakikisha aawamu ambayo Catalonia inapaswa kuwa taifa huru kwa mfumo wa kujitegemea kiutawala na mambo mengine," alisema mbele ya Bunge la Barcelona. "Ninapendekeza kusitishwa kwa mchakato huo kujitangazia uhurukwa kuanza mazungumzo ili kufikia suluhisho kupitia mazungumzo. Carles Puigdemont, hata hivyo hakuomba Bunge kuidhinishwa kwa kutangazia uhuru wa jimbo la Catalonia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana