Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Wanaharakati wa Catalonia wafikishwa mahakamani mjini Madrid

media Josep Lluis Trapero, Meja Mossos, mkuu wa Polisi wa Catalonia (katikati), kabla ya ushuhuda wake katika Mahakama ya Juu ya Uhispania Ijumaa tarehe 6 Oktoba 2017. REUTERS/Javier Barbancho

Wanaharakati wanne wanaotetea eneo la Catalonia kujitawala wamesikilizwa Ijumaa hii kwenye Mahakama ya Juu mjini Madrid (Audiencia National), nchini Uhispania.

Josep Lluis Trapero, Meja Mossos d'Esquadra, Mkuu wa polisi katika eneo la Catalonia, Teresa Laplana, kiongozi mwingine wa idara hiyo, na pia viongozi wawili wa vya vyama viwili vya kiraia, Jordi Cuixart wa shirika Omnium Cultural na Jordi Sanchez kutoka shirika la Assamblea Nacional Catalana (ANC).

Wanaharakati hawa wanakabiliwa na shutma kali: kudharau Mahakama ya Juu wakati wa kura ya maoni ya kujitawala kwa eneo la Catalonia iliyopigwa marufu. Kura ambayo ilifanyika siku ya Jumapili Oktoba 1. Wanaharakati hawa wanakabiliwa na kifungo cha mika kumi na tano jela.

Josep Lluis Trapero, Meja Mossos, mkuu wa polisi wa Catalonia, anasema wanasema walitii amri, wakati ambapo wengi wanamshtumu Mossos na mtuhumiwa mwenziye kuruhusu watu kupiga kura na kutosaidia vya kutoshakikosi cha ulinzi wa raia na polisi ya taifa.

Kwa upande wa Jordi Cuixart na Jordi Sanchez, wanakabiliwa na hukumu kubwa, kwa sababu vyama vyao ndio viliandaa maandamano yote hayo katika mji wa Barcelona na kwingineko, baada ya kushauriana. Pia wanatuhumiwa kutoheshimu maagizo ya majaji na pia kudharau mamlaka ya serikali kuu ya Uhispania.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana