Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Wanaharakati wa Catalonia wafikishwa mahakamani mjini Madrid

Wanaharakati wanne wanaotetea eneo la Catalonia kujitawala wamesikilizwa Ijumaa hii kwenye Mahakama ya Juu mjini Madrid (Audiencia National), nchini Uhispania.

Josep Lluis Trapero, Meja Mossos, mkuu wa Polisi wa Catalonia (katikati), kabla ya ushuhuda wake katika Mahakama ya Juu ya Uhispania Ijumaa tarehe 6 Oktoba 2017.
Josep Lluis Trapero, Meja Mossos, mkuu wa Polisi wa Catalonia (katikati), kabla ya ushuhuda wake katika Mahakama ya Juu ya Uhispania Ijumaa tarehe 6 Oktoba 2017. REUTERS/Javier Barbancho
Matangazo ya kibiashara

Josep Lluis Trapero, Meja Mossos d'Esquadra, Mkuu wa polisi katika eneo la Catalonia, Teresa Laplana, kiongozi mwingine wa idara hiyo, na pia viongozi wawili wa vya vyama viwili vya kiraia, Jordi Cuixart wa shirika Omnium Cultural na Jordi Sanchez kutoka shirika la Assamblea Nacional Catalana (ANC).

Wanaharakati hawa wanakabiliwa na shutma kali: kudharau Mahakama ya Juu wakati wa kura ya maoni ya kujitawala kwa eneo la Catalonia iliyopigwa marufu. Kura ambayo ilifanyika siku ya Jumapili Oktoba 1. Wanaharakati hawa wanakabiliwa na kifungo cha mika kumi na tano jela.

Josep Lluis Trapero, Meja Mossos, mkuu wa polisi wa Catalonia, anasema wanasema walitii amri, wakati ambapo wengi wanamshtumu Mossos na mtuhumiwa mwenziye kuruhusu watu kupiga kura na kutosaidia vya kutoshakikosi cha ulinzi wa raia na polisi ya taifa.

Kwa upande wa Jordi Cuixart na Jordi Sanchez, wanakabiliwa na hukumu kubwa, kwa sababu vyama vyao ndio viliandaa maandamano yote hayo katika mji wa Barcelona na kwingineko, baada ya kushauriana. Pia wanatuhumiwa kutoheshimu maagizo ya majaji na pia kudharau mamlaka ya serikali kuu ya Uhispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.