Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Mahakama Kuu yavunja kikao cha Bunge la Catalonia juu ya uhuru

Alhamisi hii Mahakama ya Uhispania imevunja kikao cha bunge kiliyopangwa kufanyika siku ya Jumatatu (Oktoba 9) katika Bunge la Catalonia kuhusu matokeo ya kura ya maoni kuhusu kujitawala kwa eneo hilo.

Wabunge wa Catalonia wanatoka bungeni baada ya kura ya azimio kwa ajili ya uhuru, tarehe 9 Novemba 2015 huko Barcelona.
Wabunge wa Catalonia wanatoka bungeni baada ya kura ya azimio kwa ajili ya uhuru, tarehe 9 Novemba 2015 huko Barcelona. REUTERS/Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Mahakama imesema iwapo kikao hicho kitaendelea wiki ijayo, hatua hiyo itakuwa kinyume cha Katiba ya nchi hiyo, wakati huu kukiwa na mvutano mkali wa kisiasa kuhusu hatima ya eneo la Catalan.

Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy ameonya uongozi wa eneo la Catalan kuacha mpango wa kutangaza uhuru wa eneo hilo kama walivyopanga kufanya.

Rajoy amesisitiza kuwa kura ya maoni iliyofanyika haikubaliki kamwe na mazungumzo yanaweza kufanyika tu iwapo, viongozi wa Catalan wataacha kutambua matokeo hayo.

Hata hivyo, kiongozi wa Catalan Carles Puigdemont amesisitiza kuwa, wiki ijayo atangaza uhuru wa eneo hilo na kuongeza kuwa haogopi kukamatwa na uongozi wa Madrid.

Misimamo kutoka pande zote mbili, inaendelea kuhatarisha hali ya kisiasa nchini humo kuelekea wiki ijayo, huku hofu ikizuka ya kutokea cha machafuko na mvutano zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.