Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Muuaji wa Marseilles atambuliwa, watu watano wakamatwa

Watu watano walikamatwa siku ya Jumanne katika mji wa Marseille, hatua muhimu ya kwanza katika uchunguzi ulioanzishwa juu ya kumtambua vema Ahmed Hanachi, raia wa Tunisia mwenye umri wa miaka 29 aliyeua wanawake wawili siku ya Jumapili kwenye kituo cha treni cha St. Charles mjini Marseille.

Katika eneo la mashambulizi, ambapo wanawake wawili ndugu waliuawa, raia wa Marseilles wamekua wakiweka shada za maua, mishumaa ya mwanga.
Katika eneo la mashambulizi, ambapo wanawake wawili ndugu waliuawa, raia wa Marseilles wamekua wakiweka shada za maua, mishumaa ya mwanga. REUTERS/Jean-Paul Pelissier
Matangazo ya kibiashara

Watu wasiopungua wanne waliokamatwa, ambao wote walikua na mawasiliano na Ahmed Hanachi, wamewekwa kizuizini kwa kosa la kushirikiana na wahalifu wa kigaidi. siku ya Jumanne jioni, chanzo kilio karibu na uchunguzi kilitangaza kukamatwa kwa mtu mwengine na mfuko wa mweusi wa muuaji wa Marseille ulipatikana wakati wa mnsako wa polisi nyumbani Ahmed Ahanchi mjini Marseilles.

Muuaji huyuambaye aliuawa wanawake wawili kwenye kituo cha treni cha Marseille siku ya Jumapili kwa kutumia kisu huku akipiga kekele akisema "Allah Akbar! "Kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa waliokua wakipiga doria, ametambuliwa rasmi kama Ahmed Hanachi, raia wa Tunisia, mwenye umri wa miaka 29, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gérard Collomb alisema Siku ya Jumanne.

"Katika miaka hivi karibuni, alikua akitembelea nchini Ufaransa katika miaka ya 2005-2006 wakati mwengine nchini Italia, inaripotiwa kuwa wakati mwingine alisema kuwa ni raia wa Morocco, Algeria au Tunisia," alieleza Waziri.

Uchunguzi unaoendelea ulitumia data ya simu ya mkononi ya muuaji, hasa kujua kama alikuwa na ndugu au jamaa nchini Ufaransa na alikuwa na uhusiano na kundi la msimamo mkali wa kidini nchini humo. Uchunguzi hasa uligundua kwamba alikuwa akisikiliza nyimbo za kidini mtandaoni, kwa mujibu wa chanzo kingine kilio karibu na uchunguzi.

Hata hivyo, madai ya kundi la Islamic State, saa chache baada ya mashambulizi, yameibua "maswali mengi" kwa sababu hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa muuaji alikua na uhusiano ua na mafungamano na kundi hilo," chanzo hicho kimesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.