Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Mfalme wa Uhispania awashtumu viongozi wa Catalonia kutishia usalama wa Uhispania

Mfalme wa Uhispania Felipe VI alitangaza siku ya Jumanne kuwa serikali inapaswa"kuhakikisha katiba inaheshimishwa", huku akiwashtumu viongozi wa Catalonia ambao "wanatarajia kutangaza uhuru wa eneo hilo kinyume cha sheria".

Mfalme wa Uhispania Felipe VI akitoa hoyuba yake kutoka Palace Royal ya Zarzuela mjini Madrid Oktoba 3, 2017.
Mfalme wa Uhispania Felipe VI akitoa hoyuba yake kutoka Palace Royal ya Zarzuela mjini Madrid Oktoba 3, 2017. Casa de SM El Rey/Francisco Gomez/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linakuha wakati maelfu ya wakazi wa mji wa Barcelona wameendelea kuandamana wakipinga vurugu zilizosababishwa na askari polisi wakati wa kura ya maoni ya kujitawala ya siku ya Jumapili. Serikali ya Uhispania ilikua ilipiga marufuku kura hiyo ya maoni.

Mvutano kati ya serikali kuu ya Uhispania na viongozi wa Catalonia wanaotishia kutangaza uhuru wa eneo hilo, unapelekea Uhispani kutumbukia katika mgogoro mkubwa tangu kurejea kwa mfumo wa demokrasia nchini humo mwaka 1977. Wakati huo huo Felipe VI aliwashtumu viongozi wa Catalonia kuwa wamejiweka kwenye nafasi ya sheria na demokrasia kwa kuandaa kura ya maoni ya Jumapili.

"Kwa maamuzi yao, viongozi wa Catalonia wamekiuka sheria zilizoidhinishwa kisheria, na hivyo kuonyesha udhalimu usiokubalika kwa Serikali. Wamevunja kanuni za kidemokrasia za utawala wa sheria na kudhoofisha amani na maisha ya kawaida katika jamii ya Catalonia. Jamii ambayo kwa bahati mbaya walifaulu kuigawa. Kwa mwenendo wao usiowajibika, viongozi wa Catalonia wanaweza hata hivyo kuhatarisha utulivu wa Catalonia na wa Uhispania nzima. Hatimaye, yote haya yalisababisha jaribio lisilokubalika katika utunzaji wa taasisi za kihistoria za Catalonia. Viongozi hawa, kwa njia wa wazi, wamejiweka kando ya sheria na demokrasia. Wanataka kuvunja umoja wa Uhispania na uhuru wa taifa, "alisema Mfalme Felipe VI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.