Pata taarifa kuu

Catalonia kutangaza uhuru wake hivi karibuni

Siku nne baada ya kura ya maoni ya kujitawala kwa eneo la Catalonia nchini Uhispania, maafisa waandamizi wa eneo hilo wamesema hivi karibuni watatangaza uhuru wa Catalonia.

Carles Puigdemont, rais wa mamlaka ya Catalonia (katikati), wakati wa kutangazwa lkura ya maoni ya kujitawala. Barcelona, 9 Juni 2017.
Carles Puigdemont, rais wa mamlaka ya Catalonia (katikati), wakati wa kutangazwa lkura ya maoni ya kujitawala. Barcelona, 9 Juni 2017. © REUTERS/Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano yake na BBC, Carles Puigdemont amesema kuwa serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo kuamua iwapo eno lao limekua huru au la.

Kauli hii inakuja wakati saa chache baada ya Mfalme wa Uhispania Felipe VI akiwashtumu viongozi wa Cataloonia kuhatarisha utulivu wa eneo hilo.

Hayo yanajiri wakati ambapo wakazi wa miji mbalimbali hasa mjini Barcelona wakiendelea na maandamano ya kupinga vurugu zilizosababishwa na polisi siku ya Jumapili wakati wa kura ya maoni ya kujitawala kwa eneo la Catalonia.

Katika makabiliano kati ya polisi na waandamanaji watu zaidi ya 850 walijeruhiwa, pamoja na polisi 33.

Licha ya Mfalme Felipe VI, kusema kuwa waandalizi wa kura hiyo walikiuka sheria, rais wa Catalonia Carles Puigdemont, amesem akuwa katiba ndio iliwaruhusu kufanya hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.