Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-USALAMA

Polisi ya Ufaransa yagundua kifaa cha kulipuka mjini Paris

Siku ya Jumatatu Oktoba 2 ofisi ya mashtaka ya Paris ilianzisha uchunguzi dhidi ya ugaidi baada ya ugunduzi usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi wiki iliyopita, mitungi minne ya gesi na kifaa cha kulipuka kiliyotengenezwa kienyeji katika tarafa ya XVI mjini Paris. Watu watano wamekamatwa.

Mitungi minne ya gesi na kifaa cha kulipuka vyaligunduliwa Paris.
Mitungi minne ya gesi na kifaa cha kulipuka vyaligunduliwa Paris. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na uchunguzi, watuhumiwa wanne walikuwa chini ya ulinzi siku ya Jumatatu jioni. Operesheni ya polisi ilifanyika katika wilaya kadhaa katika miji wa Essonne na Val-de-Marne siku ya Jumatatu, na kwa mujibu wa wenzewetu wa gazeti la kila wiki la Le Point ambalo limefichua taarifa hii, mtu aliyeorodheshwa kwa herufi kubwa ya S ni miongoni mwa watuhumiwa.

Baada ya kupewa taarifa na mtu mwema mkazi wa magharibi mwa mji mkuu wa Ufaransa, polisi iligundua mitungi minne ya gesi nne na kifaa cha kulipuka nje ya kidogo ya jengo moja. Hidrokaboni iliyokua ilisambazwa karibu na mitungi ya gesi na kifaa cha kulipuka, vikiunganishwa na simu ya mkononi na waya, pia viligunduliwa kwenye eneo hilo.

Haijafahamika lengo la wahalifu walitega vitu hivyo kwenye mlango wa jengo moja la Auteuil kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Ufaransa. Lakini maafisa wa usalama wanasema wahalifu hao walijidanganya. Wakati huo huo kitengo cha kupambana na ugaidi cha ofisi ya mashitaka ya Paris kimeanzisha uchunguzi wa "kushirikiana na wahalifu wa kigaidi", "jaribio la uharibifu kwa njia hatari inayohusiana na ugaidi" na "jaribio la mauaji yanayohusiana na ugaidi" .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.