Pata taarifa kuu
UFARANSA-KAZI

Watu zaidi ya laki mbili waandamana nchini Ufaransa

Watu 223,000 nchini Ufaransa wameandamana siku ya Jumanne Septemba 12 dhidi ya sheria ya kazi, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, wakati ambapo muungano wa vyama vya wafanyakazi wa CGT ukitangaza kwamba watu 400,000 waliitikia maandamano hayo nchini kote.

Maelfu ya waandamanaji katika mitaa mbalimbali ya mjini Paris wakipinga sheria ya kazi.
Maelfu ya waandamanaji katika mitaa mbalimbali ya mjini Paris wakipinga sheria ya kazi. REUTERS/Jean-Paul Pelissier
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Paris, makao makuu ya polisi yalihesabu waandamanaji 24,000 wakati ambapo CGT inabaini kwambawatu walioandamana walifikia 60,000.

Maandamano ya kwanza yalifanyika asubuhi. Kisha, muda mfupi kabla ya 14:30, umati wa watu waliandamana katika eneo la Bastille kuelekea eneo lililoitwa Italia.

Hayo yanajiri wakati ambapo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema anapanga kubadilisha sera ya kazi nchini humo ili kutimiza ahadi yake ya kampeni.

Macron anasema anaamini kuwa mabadiliko hayo yatasaidia kupambana na changamoto za ukosefu wa kazi nchini humo.

Mabadiliko hayo yanatarajiwa kujadiliwa bungeni na wachambuzi wanasema kuwa yatapita kjwa sababu ana wabunge wengi bungeni.

Jean-Luc Mélenchon akiongoza maandamano mjini Marseilles, Jumanne, Septemba 12, 2017.
Jean-Luc Mélenchon akiongoza maandamano mjini Marseilles, Jumanne, Septemba 12, 2017. REUTERS/Jean-Paul Pelissier

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.