Pata taarifa kuu
NORWAY-UCHAGUZI

Muungano wa kihafidhina washinda Uchaguzi Mkuu Norway

Baada kuhesabu 93.2% ya kura, muungano wa kihafidhina katika ushirika na chama cha kupambana na wahamiaji vimepata uchindi mwembamba katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumatatu. Muungano huo umepata viti 89 katika bunge kwa jumla ya viti 169.

Erna Solberg (watatu kutoka kushoto) akizungumza baada yakutangazwa matokeo ya uchaguzi wa bunge, tarehe 11 Septemba 2017 mjini Oslo.
Erna Solberg (watatu kutoka kushoto) akizungumza baada yakutangazwa matokeo ya uchaguzi wa bunge, tarehe 11 Septemba 2017 mjini Oslo. NTB Scanpix/Hans Kristian Thorbjornsen via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo serikali ijayo itakuwa dhaifu, kwa sababu chama kikuu chenye mrengo wa kati kulia na kile cha mrengo wa kushoto vinakaribiana kwa kura, kulingana na matokeo ya uchaguzi.

Bi Solberg ametawala katika ushirika na chama cha kupambana na wahamiaji.

Kampeni za uchuguzi huo mkuu zimelenga na kuzungumzia vilivyo suala la kodi, pamoja na kupunguzwa kwa ushuru kwa watunga sera ili kuongeza ukuaji wa uchumi, wakati chama cha Labour chenyewe kimejikita katika ahadi ya kuboresha huduma za umma.

Chama cha upinzani cha Labour kinaonekana kutetea nafasi yake ipasavyo kama chama kikuu katika bunge la nchi hiyo.

Muungano wa kihafidhina wa Bi Erna Solberg unawania nafasi ya kurejea madarakani kwa kipindi cha pili. Endapo atafanikiwa atakuwa ni mwanamke wa kwanza kutoka chama cha mrengo wa kulia katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kuchaguliwa katika nafasi ya waziri mkuu.

Kambi ya bii Solberg imeanza kupoteza mihula saba ikilinganishwa na mwaka 2013 lakini kura muungano wa kihafidhina ulipata zintosha kupata ushindi katika uchaguzi huu. Kamwe tangu Kåre Willoch mwaka 1985, waziri mkuu kutoka muungano wa kihafidhina hajashinda muhula wa pili mfululizo katika nchi hii yenye watu milioni 5.3. Mpinzani mkuu wa Bi Solberg, Jonas Gahr Støre alikubali kushindwa na kumpongeza mpinzani wake: "Uchaguzi huu umekata tamaa chama cha Labour," alikiri Bw Støre, mwenye umri wa miaka 57. "

Vyama vinne vinavyojumuika kwenye muungano wao wa mrengo wa kulia vimerudi nyuma, lakini bado vinashikilia idadi kubwa ya kura lakini hazina uzito wowote wa kupitisha maamuzi yoyote bungeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.