Pata taarifa kuu
USWISI-HALI YA HEWA

Watu wanane watoweka baada ya maporomoko ya udongo Uswisi

Watu wanane, ikiwa ni pamoja na raia kutoka Ujerumani, Austria na Uswisi, wanaripotiwa kutoweka kusini mashariki mwa eneo la milima la Uswisi baada ya maporomoko ya udongo ambayo yalisababisha matope mengi siku ya Jumatatu, polisi imesema Alhamisi hii.

Kijiji cha Uswisi cha Bondo baada ya maporomoko ya udongo, kwenye picha iliyotolewa tarehe 24 Agosti 2017 na polisi wa wa Grisons.
Kijiji cha Uswisi cha Bondo baada ya maporomoko ya udongo, kwenye picha iliyotolewa tarehe 24 Agosti 2017 na polisi wa wa Grisons. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Katika jimbo la Val Bondasca, watu wanane ambao walikuwapo wakati wa maporomoko hayo hawajapatikana" pmaka sasa, polisi ya mji wa Grisons imesema katika taarifa yake.

Kati ya watu hawa wanane, sita waliripotiwa kwa polisi na ndugu zao kama walitoweka. Zoezi la kuwatafuta liliendelea usiku kucha.

Kwa mujibu wa gazeti la Uswisi la Blick, ambalo linamnukuu msemaji wa polisi,mawasiliano yamekata katika mkoa huo. "Tunafikiria hii ndiyo sababu ambayo hatujaweza kuwasiliana na watu hao waliotoweka," msemaji wa polisi Markus Walser amesema.

"Kwa sasa, wataalam wa masuala ya uokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo hilo lenye milima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.