Pata taarifa kuu
UHISPANIA-IS-UGAIDI-USALAMA

Mtuhumiwa wa mwisho wa mashambulizi ya Catalonia auawa

Polisi ya Catalonia imethibitisha siku ya Jumatatu kuwa ilifanikiwa kumuua mshutumiwa wa mwisho wa mashambulizi ya wiki iliyopita katika mji wa Catalonia, mashambulizi ambayo yalisababisha vifo vya watu 15 na wengine 120 walijeruhiwa.

Gari la kubeba maiti likiegesha kwenye eneo ambapo dereva alieendesha gari lililotumiwa kwa mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu 14 katika mji wa Ramblas alipigwa risasi na polisi katika eneo la Subirats tarehe 21 Agosti 2017.
Gari la kubeba maiti likiegesha kwenye eneo ambapo dereva alieendesha gari lililotumiwa kwa mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu 14 katika mji wa Ramblas alipigwa risasi na polisi katika eneo la Subirats tarehe 21 Agosti 2017. REUTERS/Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Operesheni ya polisi iliendeshwa saa 11 jioni magharibi mwa Barcelona.

Mshutumiwa huyo alipatikana kwa msaada wa jirani yake katika eneo la Subirats, kilomita zaidi ya hamsini kutoka magharibi mwa mji mkuu Catalonia.

Vyombo vya habari vinasema mshukiwa huyo alipigwa risasi eneo la Subirats, karibu na Sant Sadurní d'Anoia na alionekana kuvalia mkanda wa kujilipua.

Polisi wamethibitisha kwamba mshukiwa huyo Younes Abouyaaqoub, raia wa Morocco mwenye umri wa miaka 22, ambaye alikuwa awali ametajwa kuwa mshukiwa aliyekuwa akisakwa kuhusiana na shambulio hilo la Las Ramblas.

Taarifa kwenye vyombo vya habari zinasema mwanamume huyo alisema kwa sauti "Allahu Akbar" ("Mungu ni mkuu") alipokabiliwa na maafisa hao.

Operesheni hiyo ya polisi ilitekelezwa maili 25 (40km) kutoka Barcelona, ambako shambulio hilo la Las Ramblas.

Abouyaaqoub alikuwa awali amedaiwa kuliteka gari hilo na kisha kuliendesha kwa nguvu kupitia kizuizi cha maafisa wa polisi na baaaye akaliacha gari hilo.

Polisi walikuwa wanashuku kwamba huenda alikuwa amefanikiwa kuingia Ufaransa.

Dereva wa gari hilo Pau Pérez, 34, kutoka Vila Franca, alipatikana ameuawa kwa kudungwa kwa kisu akiwa kwenye kiti cha nyuma cha gari hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.