Pata taarifa kuu

Ufaransa yarejesha kikosi cha polisi jamii kwa kukabiliana na ugaidi

Wizara ya mambo ya ndani ya nchini Ufaransa imetangaza kurejeshwa kwa vikosi vya polisi Jamii kama alivyokuwa ameahidi rais Emmanuel Macron wakati wa kampeni zake ambao wataitwa polisi wa usalama wa kila siku.

Ufaransa imerejesha polisi wa Jamii ambao wataitwa polisi wa usalama wa kila siku.
Ufaransa imerejesha polisi wa Jamii ambao wataitwa polisi wa usalama wa kila siku. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Paris waziri Gerard Collomb ameliambia gazeti la LE FIGARO linalochapishwa jijini humo kuwa kuna haja ya kuimarishwa ulinzi wa wananchi kuanzia ngazi za chini wakati huu kukiwa na uvumi wa kuingia kwa watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kundi linalojiita Islamic State nchini humo, wakitokea mashariki ya kati.

Kikosi hiki kiaanza kazi yake "kabla ya mwisho wa mwaka," Waziri wa Mambo ya Ndani Gérard Collomb ameliambia gazeti la Le Figaro. Na, miaka kumi na nne baada yakutoweka, kikosi hiki kitaitwa "polisi wa usalama wa kila siku".

Ni polisi ambao watakuwa na jukumu la kuwasikiliza zaidi sana raia wa kawaida wasiojiweza, kujuwa matatizo ya jamii na kuwasaidia pale inapohitajika, Bw Collomb, Waziri wa Mambo ya ndani wa Ufaransa amesema.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.