Pata taarifa kuu
UFARANSA-ULINZI

Emmanuel Macron kuongeza bajeti ya majeshi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi kuongeza bajeti ya wizara ya ulinzi ifikapo mwaka 2018. Ameitoa kauli hii siku ya alhamisi wakati akijaribu kurejesha uaminifu katika jeshi la taifa hilo baada ya kujiuzulu kwa aliekuwa mkuu wa majeshi nchini humo jenerali Pierre Villiers.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) atoa hotuba akiwa karibu na Mkuu mpya wa wa majesji ya Ufaransa, Jenerali Francois Lecointre wakati wa ziara yake katika kambi ya jeshi kusini mwa Ufaransa, Julai 20, 2017.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) atoa hotuba akiwa karibu na Mkuu mpya wa wa majesji ya Ufaransa, Jenerali Francois Lecointre wakati wa ziara yake katika kambi ya jeshi kusini mwa Ufaransa, Julai 20, 2017. REUTERS/Jean-Paul Pelissier
Matangazo ya kibiashara

Akiambatana na mkuu mpya wa majeshi jenerali François Lecointre pamoja na waaziri wa ulinzi Florence Parly, katika kituo cha kijeshi cha Istres, Emmanuel Macron amesema mwaka huu inabidi kuweka akiba, lakini kuanzia mwaka ujao badgeti ya Ulinzi pekee ndio itayo ongezwa.

Rais Macron amevitaka vikosi vya jeshi nchini humo kuangalia umuhimu wa ongezeko hilo, na kwamba hatokubali mtu yeyote yule aeleze kwamba ongezeko la badgeti linafanyika bila kujali gharama ya maisha ya vikosi vya usalama pamoja na usalama, hilo sio kweli.

Jenerali Villiers alisema alichukua hatua hiyo baada ya kutofautiana na rais Emmanuel Macron kuhusu kupunguza bajeti ya wanajeshi.

Aidha, alisema kuwa ameamua kuondoka kwa sababu hawezi kuthibitisha iwapo jeshi hilo litaendelea kuwa imara ikiwa bajeti hiyo itapunguzwa.

Wiki iliyopita, serikali ya rais Macron ilitangaza kuwa ilikuwa na mpango wa kupunguza bajeti hiyo ili kuwa chini ya kiwango kinachopendekezwa na Umoja wa Ulaya angalau kwa asilimia tatu.

Hata kabla ya kujiuzulu kwa Jenerali Villiers, rais Macron alinukuliwa na Jarida la du Dimanche akisema hatakubali uamuzi wake kutotekelezwa na kumtaka Mkuu wa jeshi hataki kushirikiana naye, basi aondoke.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.