UTURUKI-EU-USHIRIKIANO
Erdogan: Umoja wa Ulaya unatupotezea muda
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameliambia Shirika la Habari la Uigereza BBC kuwa nchi yake haitaona tatizo ikiwa ombi la nchi yake kuungana na Umoja wa Ulaya litakataliwa.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Aidha rais Erdogan amesema nchi yake inaweza kusimama peke yake na kuongeza kuwa umoja huo unaipotezea nchi yake muda.
Kiongozi huyo pia amepinga madai kuwa serikali yake imewafunga jela wanahabari 150.
Hivi karibuni Uturuki ilikumbwa na hali ya sintofahamu, siku chache tu baada ya kushundwa kwa jaribio la mapinduzi. Baada ta kisa hicho, serikali ya Erdogan iliwafunga maafisa mbalimbali wa jeshi na polisi bila kusahau maafisa wengine serikalini.