Pata taarifa kuu
UJERUMANI-MAREKANI-G20-USHIRIKIANO

Mkutano wa Hamburg kukabiliwa na mvutano

Mwezi mmoja baada ya mkutano wa nchi zenye nguvu duniani G7 katika mji wa Sicily, nchini Italia ambapo hali ya kutoelewana ilijitokeza kati ya Marekani na washirika wake kuhusu masuala ya hali ya hewa na biashara, mkutano wa G20 katika mji wa Hamburg pia unaonekana kuwa wenye mvutano zaidi.

Kansela wa Ujerumani na rais wa Marekani katika mji wa Hamburg tarehe 6 Juni, katika mkesha wa ufunguzi wa mkutano wa G20 tarehe 7 na 8 Julai 2017.
Kansela wa Ujerumani na rais wa Marekani katika mji wa Hamburg tarehe 6 Juni, katika mkesha wa ufunguzi wa mkutano wa G20 tarehe 7 na 8 Julai 2017. Steffen Kugler/Courtesy of Bundesregierung/Handout
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa nchi zilizostawi kiuchumi (G20) unazinduliwa Ijumaa hii Julai 7, 2017 ambapo watakuwepo viongozi wakuu wa nchi duniani.

Ijumaa hii katika mji wa Hamburg, kaskazini mwa Ujerumani, viongozi wa nchi zilizostawi kiuchumi duniani watakutana wakati ambao makundi ya wanaharakati yameanza kuandamana katika mji huo yakita mkutano huo wa kibepari. Makabiliano makali yanatazamiwa kutoka kati ya wanaharakati hao na vikosi vya usalama. Mkutano huu unafanyika baada ya zaidi ya miaka minane kuzuka mdororo wa kiuchumi.

Itakumbukwa kwamba kwa mujibu wa wataalam uchumi wa dunia uko sawa. ukuaji wa uchumi uko pale, ingawa bado ni dhaifu. Maendeleo makubwa yamefanywa katika mapambano dhidi ya ukwepaji kodi na udanganyifu wa kulipa kodi. Taasisi kuu ya kudhibiti mabenki ilipelekea iliruhusu kupunguza vya kutosha tishio la mdororo mpya kwa kiwango kikubwa.

IMF, Benki ya Dunia na WTO wana wasiwasi

Lakini kuwasili kwa Donald Trump katika Ikulu ay White House kumetumbukiza dunia katika mashaka. Kwanza katika nyanja ya kifedha, kwa kuwa utawala wa Donald Trump unaonekana kutojali mikakati na sheria zilizowekwa chini ya utawala wa Barack Obama, tofauti na matokeo.

Utawala wa Donald Trump pia unataka kulinda biashara yake na bidhaa kutoka Marekani na umekataa uwiano wa utandawazi ambao nchi zilizostawi kiuchumi (G20) zinataka kuendeleza. Msimamo huu wa Marekani unatia wasiwasi WTO, IMF na Benki ya Dunia, ambao wanatoa wito wa kujikita katika kuimarisha biashara duniani, na kubainisha kuwa ustawi wa mamia ya mamilioni ya watu hutegemea hivyo.

Hali ya hewa: Trump kuletwa kwenye meza ya mazungumzo

Viongozi wa Ulaya wa G20, Ijumaa hii katika mji wa Hamburg, wanatazamiwa kumshawishi rais wa Marekani Donald Trump kurejelea upya uamuzi wake wa kuiondoa nchi yake kwenye makubaliano ya kimataifa ya Paris kuhusu hali ya hewa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.