Pata taarifa kuu
UJERUMANI-USALAMA

Maandamano kuukabili mkutano wa G20 nchini Ujerumani

Ujerumani, mwaka huu ni mwenyekiti wa mataifa yaliostawi kiuchumi (G20), na Kansela Angela Merkel amechagua mji wake, Hamburg, kupokea wajumbe 35 watakaoshiriki mkutano huo, ambao utafanyika siku ya Ijumaa na Jumamosi tarehe 7 na 8 Julai.

Waandamanaji wako tayari kwa ajili ya mkutano wa G20. Hamburg, Julai 5, 2017.
Waandamanaji wako tayari kwa ajili ya mkutano wa G20. Hamburg, Julai 5, 2017. REUTERS/Wolfgang Rattay
Matangazo ya kibiashara

Kuchaguliwa kwa mji mkuu wa kaskazini mwa Ujerumani kumezua changamoto ya vifaa na salama. Mji huu kwa siku tatu kuanzia leo utakumbwa na hali ya sintofahamu.

Matukio thelathini ya maandamano yanatazamiwa kukumba mji wa Hamburg kwa kipindi chote cha mkutano. Moja ya mikusanyiko mikuu iliyoandaliwa na mrengo wa kushoto ulioitwa "Karibu kuzimu", unatarajiwa Alhamisi hii usiku.

Hamburg unakabiliwa na maandamano makubwa yaliopangwa na mrengo wa kushot. Wanaharakati kati ya 7000 na 8000 wanatarajiwa kuwasili katika mji huo, lakini pia makabiliano kati ya Wakurdi na Waturuki kufuatia kuwasili kwa rais Erdogan nchini Ujerumani. Bila kusahau tishio la ugaidi wa Kiislamu.

Maafisa 20 000 wa polisi kutoka kote Ujerumani watapelekwa katika mji wa Hamburg. Sehemu ya kuwapokelea wakimbizi,upande wa pili wa Elbe, imegeuzwa kuwa gereza lililo chini ya ulinzi mkali na lina uwezo wa kupokea hadi watu 400.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.