Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIMONE-JAMII

Simone Veil kuzikwa Jumatano hii

Siku tano baada ya kifo cha Simone Veil, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 89, sherehe rasmi ya mazishi ambayo itaongozwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron itafanyika Jumatano hii asubuhi katika makaburi ya Mashujaa.

Simone Veil Machi 18, 2010.
Simone Veil Machi 18, 2010. François Guillot/AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi mbalimbali barani Ulaya na nchini Ufaransa watatoa heshima ya mwisho kwa waziri huyo wa zamani, alietunga sheria inayoruhusu kutoa mimba nchini Ufaransa .

Emmanuel Macron ataongoza sherehe ya mazishi. Rais Macron atatoa hotuba fupi inayoelezea maisha ya Simone Veil, hususan kupelekwa kwa waziri huyo wa zamani wa Ufaransakatika kambi ya Auschwitz wakati wa Vita Kuu ya pili, ahadi yake kwa Ulaya na dhamira yake kwa wanawake iliyompelekea kupitisha sheria inayohalalisha utoaji mimba mnamo mwaka 1975.

Kwa upande wa serikali, Mawaziri wakuu kadhaa wa kigeni watahudhuria sherehe ya mazishi. Miongoni mwao, Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel, Waziri Mkuu wa Luxemburg na Waziri Mkuu wa Bulgaria Boiko Borissov. Marais wa tatu wa zamani wa Ufaransa Valery Giscard, nicolas Sarkozy na François Hollande watahudhuria sherhe hiyo.hali Hali ya afya ya Jacques Chirac haimruhusu kwenda kwenye makaburi ya Mashujaa, kwa mujibu wa gazeti la Journal de dimanche. Atawakilishwa na mkewe Bernadette na binti yao Claude.

Wanasiasa wengi wa Ufaransa, viongozi wa sasa au wa zamani wa taasisi za Ulaya pia wanatarajiwa kuhudhuria sherehe ya mazishi ya Simone Veil.

Sherehe itaanza saa 10:30 ( saa za Ufaransa).

Tangu kifo chake siku ya Ijumaa iliopita, rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali Ulaya na nchini Ufaransa zimekua zikitolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.