Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Viongozi wa dunia wamkumbuka Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl

Viongozi mbalimbali wa dunia wametoa heshima zao za  mwisho kwa Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl aliyefariki dunia mwezi uliopita.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akitoa heshima za mwisho kwa  aliyekuwa Kansela wa nchi hiyo Helmut Kohl, katika bunge la Umoja wa Ulaya Julai 1 2017
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Kansela wa nchi hiyo Helmut Kohl, katika bunge la Umoja wa Ulaya Julai 1 2017 ©REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Kohl amekumbukwa kama kiongozi shupavu, aliyefanikiwa kuliunganisha taifa la Ujerumani lakini pia kuhamasisha Umoja wa Ulaya miaka ya tisini.

Jeneza lililobeba mwili wake, lilifunikwa na bendera ya Umoja wa Ulaya.

Hii ndio mara ya kwanza kwa Bunge la Umoja wa Ulaya kuwa na msiba wa Umoja huo na mwili wa kiongozi wa Ulaya kuwekwa ndani ya bunge hilo lenye makao yake mjini Strasbourg nchini Ufaransa.

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, Kansela wa sasa wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria ibada hiyo.

Kansela akiwa mwenye hisia, amesema kuwa kama sio kazi kubwa ya Kohl, maisha ya Mamilioni ya Wajerumani yasingebadilika na kuwa kama yalivyo sasa.

Naye rais Macron amesema, Kansela huyo wa zamani alikuwa ni rafiki wa karibu na wa dhati wa Ufaransa.

Kiongozi huyo wa zamani alifariki dunia mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 87.

Aliiongoza  Ujerumani  kati ya mwaka 1982-1998.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.