Pata taarifa kuu
UINGEREZA-MOTO

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mkasa wa moto nchini Uingereza yafikia 17

Maafisa wa zima moto jijini London nchini Uingereza wamekuwa wakipambana usiku kucha kuzima moto katika jengo la orofa 24 lililoteketea siku ya Jumanne usiku.

Jengo la grenfell lilivyoteketea kwa moto
Jengo la grenfell lilivyoteketea kwa moto Daniel LEAL-OLIVAS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa, Polisi wamethibitisha kuwa watu 17 wamepoteza maisha huku wengine wakiendelea kupokea matibabu katika hospitali mbalimbali.

Mambo muhimu tunayofahamu kuhusu kuteketea kwa jengo hili la Grenfell Tower:-

  • Polisi inahofia kuwa idadi ya vifo itaongezeka.
  • Watu 70 wanatibiwa katika hospitali mbalimbali, 18 wako katika hali mbaya.
  • Majina ya watu waliopoteza maisha yameanza kutolewa.

Waziri Mkuu Theresa May ametangaza kuwa uchunguzi mahsusi utafanyika kubaini chanzo cha moto huo.

Kufikia siku ya Alhamisi, moshi umeendelea kuonekana katika jengo hilo huku Polisi wakisema kuwa watu 65 waliokolewa wakiwa hai.

Waziri Mkuu May amechelewesha kuunda kwa serikali ya pamoja kutokana na mkasa huo wa moto.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.