Pata taarifa kuu
UINGEREZA-SIASA

Hakuna chama kitakachopata ushindi wa kuunda serikali nchini Uingereza

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu nchini Uingereza yanaonesha wazi kuwa hakuna chama kitakachopata ushindi katika Uchaguzi wa wabunge uliofanyika siku ya Alhamisi ili kuunda serikali peke yake.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May baada ya kuonekana siku ya Ijumaa Juni 9 2017
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May baada ya kuonekana siku ya Ijumaa Juni 9 2017 REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Hili ni pigo kwa Waziri Mkuu Theresa May aliyeitisha Uchaguzi wa mapema, akiamini kuwa atapata uungwaji mkono na kuaminiwa, ili kuongoza serikali peke na kuepusha serikali ya muungano.

Inatarajiwa kuwa chama cha Conservative kinatarajiwa kupata ushindi wa viti 318, huku kile cha Labour kikitarajiwa kupata 262.

Waziri Mkuu May amesema baada ya matokeo ya mwisho kutangazwa, kutakuwa na muda wa udhabiti huku kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn akimtaka May, ajiuzulu.

Chama cha Labour kimeonekana kuongeza viti bungeni, huku Conservative kikipoteza.

Conservative kilihitaji kupata viti 326 ili kuongoza serikali peke yake lakini kwa namna mambo yalivyo, itabidi kupata uungwaji mkono kutoka chama kingine ili kuunda serikali.

Haijafahamika ikiwa, Bi.May ataendelea kuongoza chama hicho kutokana na matokeo haya mabaya, kinyume na matarajio yake.

Kazi kubwa, iliyo mbele ya serikali mpya itakayoundwa ni kuendeleza na kufanikisha mchakato wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Mambo muhimu kuhusu uchaguzi wa Uingereza:

  • Chama kilicho na idadi kubwa ya viti ambavyo ni 326 kati ya 650 ndicho kinachounda serikali.
  • Chama kikishindwa kupata idadi inayohitajika kuunda serikali, inahitaji kuingia katika mazungumzo na vyama vingine kupata idadi inayohitajika.
  • Ikiwa juhudi za kupata idadi kubwa ya vita itashindikana, basi Waziri Mkuu aliye madarakani ataendelea kuongoza hadi pale chama kitakachokuwa tayari kufanya hivyo kitajitokeza.
  • Kikao cha kwanza, kinatarajiwa kufanyika tarehe 13 mwezi Juni huku Malkia Elizabeth wa pili akitarajiwa kulifungua rasmi tarehe 19 mwezi Juni.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.