Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Vladimir Putin kuzuru Versailles

media Emmanuel Macron ameonya kwamba atatoa hotuba kuhusu Ukraine wakati wa ziara ya rais wa Urusi , mjini Versailles, Ufaransa. REUTERS/Philippe Wojazer

Rais wa Ufaransa anatarajia kumpokea Jumatatu hii, Mei 29 mwenzake wa Urusi kwa ziara ya kiserikali. Mkutano kati ya Vladimir Putin na Emmanuel Macron utafanyika katika mji wa Versailles, makazi ya Wafalme Louis XIV, Louis XV na Louis XVI.

Viongozi hao wawili watazindua katika eneo la Grand Trianon maonyesho kuhusu Pierre lw Grand, Mfalme wa wananchi wote wa Urusi.

Miaka 300 iliyopita, mahakama ya mjini Versailles ilimpokea Pierre le Grand, alipokua katika ziara yake kuelekea Ulaya. Ulaya ambayo marais wa Urusi na Ufaransa wanaichukulia leo kila mmoja kwa mtazamo wake. Rais wa Urusi anaiona kama chombo dhaifu kisichokuwa na uhuru, nae rais wa Ufaransa amejipa ahadi ya kuirejesha upya Ulaya katika hadhi yake.

Moscow haijauzungumzia kuhusu ushinda wa Emmanuel Macron. Vladimir Putin alikua na mahusiano mazuri na François Fillon. Alikiona katika chama cha National Front kama ni chama kinachotetea utaifa na kupambana dhidi ya Ulaya. Katikati mwa duru mbili za uchaguzi, na hata baada ya duru hizo, vyombo vya habari vya Urusi viliendesha kampeni ya uchochezi dhidi ya Emmanuel Macron, alisema mwandishi wetu katika mji wa Moscow, Muriel Pomponio.

Emmanuel Macron amechukulia tukio hili la kihistoria na kitamaduni kuimarisha uhusiano wa diplomasia. Nae Vladimir Putin, mwaliko kwa kuzuru mji wa Versailleshangeweza kuukataa. Mwaliko huu unachukua nafasi ya mkutano kati ambao haukufanyika kati ya François Hollande na rais wa Urusi Vladimiri Putin mnamo mwezi Oktoba kwa uzinduzi wa kituo cha utamaduni wa Urusi mjini Paris.

Rais wa Urusi anaihitaji Ulaya. Harakati zake dhidi ya Ulaya hazikuipeleka Urusi mahali popote, na mahusiano na Donald Trump yanatiliwa mashaka. Vladimir Putin na Emmanuel Macron walipigiana simu tarehe 18 Mei, kwa jitihada za Moscow.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana