Pata taarifa kuu
UFARANSA

Rais Macron achelewesha hatua ya kulitaja Baraza lake la Mawaziri

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron  ameahirisha hatua ya kulitaja Baraza lake la kwanza la Mawaziri hadi siku ya Jumatano.

Waziri Mkuu Edouard Philippe akiwa na rais Emmanuel Macron
Waziri Mkuu Edouard Philippe akiwa na rais Emmanuel Macron rfi
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa imepangwa kuwa Baraza hilo litajwe leo lakini Ikulu jijini Paris imesema  hatua hii imechukuliwa ili kumaliza uchunguzi wa Mawaziri wanaotarajiwa kuteuliwa.

Ripoti zinasema kuwa, kinachochunguzwa ni rekodi yao ya ulipaji kodi lakini pia kuthathmini ikiwa watakuwa na maslahi binafsi ikiwa watapewa nafasi hizo.

Pamoja na hilo, wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema kuwa rais Macron anahitaji muda zaidi kuhakikisha kuwa Baraza lake linakuwa na uwakilishi wa pande zote za kisiasa.

Rais huyu mpya mwenye umri wa miaka 39, aliahidi kuunda serikali itakayowaleta pamoja wanasiasa wa Republican na Kisosholisti katika harakati za kuliunganisha kisiasa taifa hilo.

Macron ni rais aliyechaguliwa akiwa na msimamo wa kati, asiyeegemea siasa za mrengo wa kulia wala kushoto.

Siku ya Jumatatu, alimteua Edouard Philippe mwenye umri wa miaka 46 kuwa Waziri wake Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.