Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Rais Trump aungana na viongozi wengine wa Dunia kumpongeza rais mpya wa Ufaransa

Rais wa Marekani Donald Trump, ameungana na viongozi mbalimbali wa dunia kumtumia salamu za pongezi  rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron baada ya kushinda uchaguzi wa duru la pili uliofanyika Mei 7 mwaka huu.

Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron REUTERS/Jean-Paul Pelissier
Matangazo ya kibiashara

"Hongera sana kwa Emmanuel Macron kwa kuchaguliwa kuwa rais ajaye wa Ufaransa, natarajia kushirikiana naye," ameandika rais Trump katika ukurasa wake wa Twitter.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa dunia kupongeza ushindi wa Emmanuel Macron dhidi ya Marine Le Pen.

Theresa May amesema kuwa Ufaransa ni mshirika wa karibu wa Uingereza na kwamba nchi yake itahakikisha inafanyakazi kwa karibu na Emmanuel Macron kama rais mpya wa Ufaransa.

Kwa upande Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amepongeza ushindi wa Macron ma kusema kuwa ushindi huo ni ushindi wa nchi za Umoja wa Ulaya.

Naye waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujerumani amesema kuwa ushindi wa Macron unapaswa kuungwa mkono na Ulaya kwa kuwa unaibakiza Ufaransa katika moyo na kitovu cha Umoja wa Ulaya.

Rais wa Ufaransa anayemaliza muda wake amepongeza ushindi huo kwa kusema ni ushindi unaolenga kulinda maslahi ya wananchi wa Ufaransa.

Rais wa Tume ya Ulaya Juncker amewapongeza wapiga kura wa Ufaransa kwa kuchagua mtu ambaye anatambua umuhimu wa Umoja wa Ulaya na mustakabali wa baadaye wa Umoja huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.