Pata taarifa kuu
UCHAGUZI UFARANSA 2017

Baada ya kuchaguliwa Macron asema atakuwa rais wa wananchi wote

Matokeo ya rasmi ya uchaguzi mkuu wa duru ya pili nchini Ufaransa yametangazwa ambapo mgombea mwenye msimamo wa kati kutoka vuguvugu la En Marche Emmanuel Macron ameshinda kwa kupata asilimia 66.1 dhidi ya asilimia 33.9 alizopata Marine Le Pen.

Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron Fuente: Ministerio del Interior francés
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine rais mteule Emmanuel Macron amewashukuru raia waliompigia kura na kumfanya awe rais wao, ambapo ameahidi kuwaunganisha raia wote na kulipigania taifa lake.

Akizungumza kutoka kwenye makao yake makuu ya kampeni, Macron amesema anatambua jukumu kubwa lililoko mbele yake na kwamba atahakikisha anapigania haki za raia wote bila kubagua.

Macron pia ametoa shukrani kwa wapiga kura ambao hawakumpigia kura akisema wametekeleza haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi waliyemtaka ambapo amesema licha ya yote hayo bado anawaona ni raia wa Ufaransa na wanastahili kusikilizwa.

Macron amesema jukumu lililoko mbele yake ni kuhakikisha analinda maslahi ya taifa ya Ufaransa kwenye umoja wa Ulaya na kwamba kama alivyoahidi wakati wa kampeni anataka kuona Ulaya mpya chini ya uongozi wake.

Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza kwenye makao makuu ya kituo cha kampeni kuwashukuru wananchi. May 7, 2017
Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza kwenye makao makuu ya kituo cha kampeni kuwashukuru wananchi. May 7, 2017 REUTERS/Lionel Bonaventure/Pool

Kuhusu huduma za kijamii Macron amesema anatambua changamoto za kijamii zilizoko ikiwa ni pamoja na hali tete ya uchumi na tatizo la ukosefu wa ajira nchini matatizo aliyosema anatambua namna ambavyo wananchi wamechoshwa na hali ya mambo ilivyo.

"Jukumu langu la kwanza ni kuhakikisha nawaunganisha raia wote wa Ufaransa bila ya kujali mirengo ya kisiasa wanayotoka, kwani taifa hili ni taifa la watu wote." alisema Macron.

Muda mfupi uliopita Marine Le Pen amewahutubia wafuasi wake na kutangaza kumpongeza Macron kwa ushindi alioupata huku akisema uchaguzi huu umekuwa ni wa kihistoria.

Le Pen amesema matokeo haya yametoa taswira mpya kwa siasa za Ufaransa ambapo amewashukuru wapiga kura wake kwa kumuunga mkono toka kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa yeye ataongoza upinzani bungeni ili katika kuhakikisha nchi yao inarejea kwenye ramani ya dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.