Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Wakuu wa nchi za EU wanakutana kujadili Uingereza kujitoa kwenye umoja wao

media Rais wa baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk, waziri mkuu wa Sweden Stefan Lofven, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri mkuu wa Slovenia Miro Cerar wakati walipokutana hivi karibuni. REUTERS/Dylan Martinez

Wakuu wa nchi kutoka jumuiya ya umoja wa Ulaya wanatarajia kuonesha mshikamano wao wakati wa mkutano wao Jumamosi hii ambapo wataidhinisha mpango wa maelekezo ya miaka miwili kwa nchi ya Uingereza kujitoa kwenye umoja huo.

Wakuu hao kutoka nchi 27 zilizosalia wanatarajiwa kuitaka Uingereza kutatua masuala muhimu kuhusu kujitoa kwake kunakohusu watu, fedha na Jamhuri ya Ireland kabla ya kufanyika kwa mazungumzo yoyote ya baadae.

Mkutano huu unafanyika huku joto la kujitoa kwa Uingereza likiwa linapanda pamoja na vita ya meneno kati ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May kuhusu majadiliano.

Rais wa umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema kwenye barua yake kwa wakuu hao wa nchi kuwa “kabla ya kujadili mustakabali wa baadae, ni lazima kwanza tutatue tofauti zetu za zamani” akiwapa wito wa kuungana kwenye masuala ya msingi.

Viongozi hao pia wanatarajia kuunga mkono wazo wa nchi ya Ireland Kaskazini kuwa mwanachama wa umoja huo ikiwa itaungana na Ireland na kuitaka Uhispania kuwa na usemi kuhusu athari za eneo la Gibraltar.

Viongozi hawa pia kwa mara ya kwanza watajadili athari za Uingereza kujitoa, makao mapya ya benki za Ulaya ambazo kwa sasa zina makao jijini London.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana