Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Mambo muhimu kuhusu Uchaguzi Mkuu nchini Ufaransa

Wakati Wafaransa Milioni 47 wakipiga kura kumchagua rais mpya siku ya Jumapili, fahamu mambo muhimu kuhusu Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Wagombea urais nchini Ufaransa
Wagombea urais nchini Ufaransa Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa nini uchaguzi huu ni muhimu?
Uchaguzi huu ni muhimu kwa sababu taifa la Ufaransa ni taifa la pili kwa nguvu za kiuchumi Barani Ulaya na pia ni moja ya mataifa yenye nguvu za kijeshi duniani.

Pia uchaguzi huu unaweza kutikisa Umoja wa Ulaya kwa kuwa wagombea wawili kati ya wanne wanaopewa nafasi,  wanakwenda kinyume na umoja huo na hata kuna hofu kuwa matokeo ya uchaguzi huo yanaweza kuchagiza Ufaransa kujitoa katika Umoja Ulaya kama ilivyokuwa kwa Uingereza.

Ni namna gani rais wa Ufaransa huchaguliwa?

Rais wa Ufaransa huchaguliwa moja kwa moja na wapiga kura kupitia kisandu cha kura ndani duru moja ya uchaguzi au duru mbili kama hakutakua na mgombea atakayeshinda moja kwa moja kwa asilimia 50.

Kama hakutakuwa na mgombea aliyeshinda katika duru ya kwanza, uchaguzi wa duru ya pili hufanyika baada ya wiki mbili na mfano mzuri ni uchaguzi wa mwaka huu duru ya kwanza ni April 23 na duru ya pili mwezi Mei tarehe 7.

Hata hivyo historia inaonyesha kuwa tangu mwaka 1965 chaguzi zote zimekuwa zikiingia katika duru ya pili .

 

 

 

Ni wagombea gani wako katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa Ufaransa mwaka huu?

Katika Uchaguzi wa Mwaka huu kuna wagombea 11.  Kutoka mrengo wa kushoto,  mrengo wa mbali kulia lakini katika hao kuna wagombea Marine Le Pen, umri wa miaka  48, Emmanuel Macron, 39, Francois Fillon, 63, na Jean-Luc Melenchon, 65.

Wagombea wengine wanaoshiriki katika uchaguzi huo ni Benoit Hamon, 49, Philippe Poutou 50, Nicolas Dupont-Aignan, 56, Francois Asselineau, 59 , Jacques Cheminade, Nathalie Arthaud, 47 na Jean Lassalle, 61.

Uchaguzi wa Ufaransa hufanyika namna gani?

Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna wapiga kura milioni 46.87 waliojiandikisha kupiga kura huku kukiwa na vituo 66,546 nchi nzima.

Watu hupiga kura kuanzia saa mbili kamili sas za Ufaransa.

Hata hivyo katika miji mikubwa kama Paris na mingine vituo vya Kupigia kura vitakua wazi mpaka saa mbili usiku.

Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kufanyika huku kukiwa na hali ya hatari kufuatia tishio la mashambulizi kigaidi.

Askari polisi wapatao 50,000 wakisaidiwa na wanajeshi 7,000 watakuwa wakipiga doria wakati na baada ya uchaguzi ili kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.

Matokeo ya uchaguzi yataanza kutolewa muda gani?

Matokeo ya awali ya Uchaguzi huo yanatarajiwa kuanza kutolewa saa mbili Usiku kwa saa za Ufaransa.

 

Inachukua muda gani rais kuapishwa ?
Kama duru ya pili itafanyika Mei 7 kama inavyotarajiwa, basi rais mpya ataapishwa ndani ya wiki moja mpaka kufikia Mei 14 ambayo ndiyo siku ya mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.