Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Malkia Elizabeth II kuadhimisha miaka 91

media Elizabeth II, Malkia wa Uingereza, hapa katika mji wa Plymouth, mwezi Machi mwaka 2015. REUTERS/Matt Cardy/Pool

Malkia Elizabeth II, ambaye anaadhimisha miaka 91 Ijumaa hii Aprili 21, ameagiza wajumbe wengine kutoka familia yake ya kifalme kumuwakilisha katika mamlaka yake mengine. Lakini afya ya kiongozi huyo kongwe nchini Uingereza inaendelea kuzorota.

Kama kila mwaka, siku ya kuzaliwa ya Malkia, itasheherekewa huku mizinga 41 ikipigwa katika Hyde Park na mingie 62 katika mnara wa London.

Malkia Elizabeth II ambaye alizaliwa Aprili 21, 1926, huwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa katika hatua mbili: katika tarehe ambayo alizaliwa, na katika sherehe rasmi ya mwezi Juni, kulingana na mila za kale na lengo la kuepuka machafuko ya hali ya hewa .

"Bado niko hai," alisema Malkia miezi miwili iliyopita wakati wa ziara yake nchini Ireland ya Kaskazini.

Itafahamika kwamba Malkia Elizabeth II ametimiza miaka 65 akiwa kiti cha enzi nchini Uingereza.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana