Pata taarifa kuu

Hollande kuitisha baraza la Usalama siku moja baada shambulizi

Rais wa Ufaransa François Hollande ameuitisha mkutano wa baraza lake la masuala ya usalama, Ijumaa asubuhi siku moja baada ya shambulizi la kigaidi kutokea kwenye mtaa wa Champs Elysées mjini Paris na kugharimu maisha ya polisi mmoja na kuwajeruhi wengine wawili.

Rais wa Ufaransa François Hollande ameahidi kuitisha mkutano wa baraza lake la masuala ya usalamasiku moja baada ya shambulizi lililogharimu maisha ya olisi mmoja Paris.
Rais wa Ufaransa François Hollande ameahidi kuitisha mkutano wa baraza lake la masuala ya usalamasiku moja baada ya shambulizi lililogharimu maisha ya olisi mmoja Paris. AFP/Philippe Desmazes
Matangazo ya kibiashara

François Hollande ametoa salamu za rambirambi kwa familia za waathirika wa mashambulizi na kuahidi ushirikiano na kuwahakikishia huduma za usalama.
Risasi zilipigwa kwenye saa tatu usiku siku ya Alhamisi, April 20 kwenye mtaa wa Champs Elysées mjini Paris, nchini Ufaransa. Polisi mmoja aliuawa, wengine wawili walijeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, mshambulizi aliuawa kwa risasi. viongozi wanaona kwamba shambulio hilo ni la kigaidi.

Milio ya risasi ilisikika katika Ikulu ya Champs Elysées. Inaamika kuwa mshambuliaji au washambuliaji walifyatua risasi kwa silaha za kivita dhidi ya gari la polisi lililokua limeegeshwa katika moja ya mtaa wa mji wa Paris.

Polisi mmoja aliuawa na wingine wawili kujeruhiwa, yamearifu makao makuu ya polisi ambayo yanaomba raia kuepuka kutembelea eneo linalozingirwa na vikosi vya usalama.

Hata hivyo polisi iliingilia kati na kufaulu kumuua mshambuliaji, imesema Wizara ya Mambo ya Ndani. Bado ni vigumu kwa sasa kujua hali halisi ya mambo kuhusiana na tukio hilo. Kwa saas polisiimezingira eneo latukio na bado inawatafuta washambuliaji wengine.

Kundi la Islamic State limedai Alhamisi hii usiku kwa njia yachombo chake cha propaganda Amaq kwa limehusika na shambulio katika mtaa wa Champs Elysées ambapo polisi aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa vibaya, huku mshambuliaji akiuawa kwa kupigwa risasi.

Kutokana na tukio hilo wagombea urais 11 wameonyesha kuguswa na tukio hilo.

Mgombea mwenye msimamo wa kati Emmanuel Macron na mwenzake mwenye wa mrengo wa kushoto François Fillon kwa pamoja walitoa heshima zao na pole kwa askari aliyeuawa wakati wa makabiliano ya jijini Paris.

Macron amesema “jukumu la kwanza la rais ni kuwalinda raia” huku Fillon akisema ataahirisha kampeni zake za Ijumaa hii ambayo ndio siku ya mwisho ya kampeni.

Mgombe Marine Le Pen pia ametangaza kuahirisha kampeni zake za mwisho kutokana na tukio hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.