Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Jaribio la mashambulizi lazimwa siku 5 kabla ya uchaguzi wa urais Ufaransa

Watu wawili wenye msimamo mkali wanaotuhumiwa kuandaa mashambulizi makubwa nchini Ufaransa wamekamatwa jumanne hii Aprili 18 katika mji wa Marseille. Taarifa hii imethibitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Matthias Fekl baada ya kukamatwa kwa watu wawili wenye umri wa miaka 23 na 29.

Vikosi vya usalama vyatumwa kwa wingi katika maeneo kulikofanyika msako, Aprili hii 18.
Vikosi vya usalama vyatumwa kwa wingi katika maeneo kulikofanyika msako, Aprili hii 18. Boris Horvat/AFP
Matangazo ya kibiashara

 Rais Francois Hollande amekaribisha hatua hiyo ya kukamatwa kwa watu hao.

Watu hao wawili wamekamatwa, siku tano kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, shirika la habari la AFP limearifu likinukuu vyanzo vilio karibu na uchunguzi.

Wawili hao "wanatuhumiwa kutaka kuchukua hatua kutekeleza mashambulizi makali," chanzo kimoja kimesema. Walikamatwa na maafisa wa usalama wa taifa kwa minajili ya uchunguzi kwa kosa la kushirikiana na wahalifu wa kigaidi. Kesi hiyo imefunguliwa mjini Paris.

Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuwa washukiwa waliokamatwa walikuwa na mpango wa kufanya mashambulizi "katika siku chache zijazo." Matthias Fekl pia amekumbusha kwamba polisi 50,000 watapelekwa kwa kila moja ya duru mbili za uchaguzi wa urais mnamo tarehe 23 Aprili na 7 Mei

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.