Kampeni za urais nchini Ufaransa zaingia kipindi cha lala salama
Ni wiki moja kamili kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa urais nchini Ufaransa tarehe 23 mwezi huu wa Aprili.
Imechapishwa:
Kampeni zimeingia katika dakika za lala salama, huku wagombea wakisalia na siku chache kunadi sera zao mbele ya rais wa Ufaransa ambao Jumapili ijayo watapiga kura, kuamua ni nani atakuwa rais wao.
Uchaguzi wa Jumapili ijayo, utakuwa ni wa awamu ya kwanza. Mshindi anahitaji kupata thuluthi mbili ya kura zote ili kutangazwa mshindi.
Hata hivyo, inavyoonekana kutakuwa na duru ya pili ya Uchaguzi huo tarehe 7 mwezi Machi.
Rais wa sasa Francois Hollande hawatania tena, uamuzi ambao aliufanya mwezi Desemba mwaka uliopita.
Kati ya wagombea 11 wanaotafuta urais, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa ushindani mkali utakuwa kati ya Marine Le Pen, Emmanuel Macron, Francois Fillion na Benoit Hammon.