Pata taarifa kuu
SYRIA

Mataifa ya G7 yataka Urusi kuacha kuiunga mkono serikali ya Syria

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Mataifa saba ya G7 yaliyoendelea kiviwanda wanaokutana mjini Lucca nchini Italia wanathathmini mbinu za kuishawishi Urusi kuacha kumuunga mkono serikali ya Syria inayoongozwa na rais Bashar Al Assad.

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Matifa ya G7 nchini Italia.
Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Matifa ya G7 nchini Italia. REUTERS/Max Rossi
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson, amesema kuwa huenda Urusi ikawekewa vikwazo ikiwa itaendelea kuiunga mkono serikali ya Syria ambayo imeshtumiwa kutekeleza shambulizi la silaha za kemikali na kusababisha vifo vya raia wa kawaida zaidi ya 70 mkoani Idlib.

Mkutano huu wa Jumanne unakutanisha pia Mawaziri kutoka Uturuki, Saudi Arabia, Milki za Kiarabu, Jordan na Qatar mataifa ambayo yanapinga utawala wa Assad.

Wakati uo huo, Waziri wa Ulinzi James Mattis wa Marekani amewaambia Mawaziri hao kuwa shambulizi la nchi yake katika uwanja wa ndege nchini Syria wiki iliyopita, liliharibu ndege za kivita za serikali ya Damascus.

Aidha, amesema kuwa Marekani haitavumilia tena matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya raia wa Syria.

Naye Waziri wa nje wa Marekan Rex Tillerson anatarajiwa kwenda jijini Moscow nchini Urusi kukutana na mwezake Sergei Lavrov na kuzungumzia kwa kina shambulizi hilo na mzozo wa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.