Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Uingereza: Waziri mkuu Theresa May atia saini barua rasmi kujitoa EU

media Picha ya Serikali ya Uingereza ikimuonesha waziri mkuu Theresa May akitia saini barua rasmi ya kujitoa kwenye umoja wa Ulaya. Machi 28, 2017 REUTERS/Christopher Furlong/Pool

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May hatimaye ametia saini barua ya kihistoria ambayo itashuhudia nchi hiyo ikianza rasmi mchakato wa kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya wakati huu pia akitoa wito wa umoja hata baada ya nchi ya Scotland kupiga kura kuitisha kura mpya ya maoni kuhusu kujitenga na Uingereza.

Serikali ya Uingereza Jumatano ya wiki hii itaiwasilisha barua hiyo kwa rais wa umoja wa Ulaya Donald Tusk, kumtaarifu rasmi kuhusu nia ya nchi hiyo kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya baada ya miaka 44 ya uanachama.

Wakati atakapolihutubia bunge juma hili waziri mkuu May atakubali kuwa kura ya kujitoa ya mwezi Juni mwaka jana ilikuwa wakati mgumu sana kwao lakini ataeleza matumaini ya nchi hiyo kutotetereka hata baada ya kujitoa.

“Sisi ni watu wamoja wenye nguvu na taifa lenye historia ya kujivunia na mustakabali mzuri wa baadae. Na sasa wakati uamuzi umefanyika kujitoa kwenye umoja wa Ulaya, ni muda wa kuja pamoja,” atasema hivyo waziri May kwenye hotuba ambayo imechapishwa awali kwenye tovuti ya Serikali.

Rais wa Umoja wa Ulaya, Donald Tusk. REUTERS/Remo Casilli

Hotuba yake ataitoa ikiwa ni saa chache tu zimepita toka wabunge kwenye nchi ya Scotland waunge mkono pendekezo la waziri wa kwanza Nicola Sturgeon aliyetaka kufanyike kura nyingine ya maoni kuhusu kujitoa kwenye umoja wa Ulaya.

Waziri mkuu May amesema kuwa wakati huu haukuwa wakati wa Scotland kufanya kura nyingine ya maoni, lakini wabunge wa Scotland wamekaidi wito wake ambapo wabunge 69 waliunga mkono kati ya wabunge 59 waliopinga kufanyika kwa kura hiyo.

Sturgeon sasa anatarajiwa kuandika barua rasmi kuomba kura hiyo ifanyike, kura ambayo anasema itafanyika mwaka 2019 kabla ya Uingereza kujitoa kwenye umoja wa Ulaya rasmi kura itakayoamua ikiwa Scotland itaendelea a unachama wake kwenye umoja wa Ulaya.

Hata hivyo kwa kura hii kufanyika, waziri Sturgeon atahitajika kuitaarifu Serikali ya Uingereza ili iweze kutoa kibali cha kura hiyo kufanyika, lakini hata hivyo tayari Serikali imeshaonesha dalili kuwa haiungi mkono kura hiyo kufanyika wakati huo,

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana