Pata taarifa kuu
UJERUMANI-MAREKANI-NATO_USHIRIKIANO

Berlin yafutilia mbali shutuma za Donald kuhusu Nato

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amefutilia mbali Jumaili hii Machi 19 madai ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyotoa siku moja kabla kwenye twiter, akisema kuwa Ujerumani inakabiliwa na mzigo wa deni wa kiasi kikubwa cha fedha kwa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) na Marekani, kutokana na gharama za kijeshi zisizotosha.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Ursula von der Leyen, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, Juni 4, 2014.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Ursula von der Leyen, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, Juni 4, 2014. REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump aliinyooshea kidole Ujerumani chini ya masaa 24 baada ya mkutano Kansela Angela Merkel kukutana na rais wa Marekani mjini, mkutano ambao ulifanyika katika furaha isio kuwa ya kawaida.

"Hakuna akaunti ambayo yameorodheshwa madeni katika NATO," amesema Ursula von der Leyen, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, akijibu kauli ya rais wa Marekani aliyoitoa siku moja kabla.

Donald Trump aliinyooshea kidolea cha lawama Berlin, akiishutumu kuwa ina deni la kiasi kikubwa cha fedha kwa NATO na kuitolea wito Ujerumani kulipa zaidi kwa ajili ya ulinzi "mkubwa na wa ghali " iliyotolewa. Hata hivyo, Kansela wa Ujerumani, mapema katika mahojiano yake na rais wa Marekani, alijikubalisha kuheshimu ahadi ya NATO ya mwaka 2014, ambayo ni kuongeza matumizi ya kijeshi hadi 2% ya Pato la la Ndani la Taifa katika muda wa miaka 10.

Nchi 5 tu kati ya wanachama 28 wa NATO zimeikia ngazi hii. Hata hivyo Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amesema kuwa ongezeko la bajeti haihusu tu NATO, lakini pia inahusu tume za amani katika mfumo wa Umoja wa Mataifa, tume za Ulaya na mapambano dhidi ya kundi la Islamic. Ursula von der Leyen ameongeza kuwa ilikuwa ni muhimu kwa kugawana sawa gharama kati ya wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.