Pata taarifa kuu
UFARANSA-MACRON-MERKEL-SIASA

Emmanuel Macron afurahia mkutano wake na Angela Merkel

Emmanuel Macron amekutana na Angela Merkel Alhamisi hii Machi 16 katika Ofisi ya Kansela huyo wa Ujerumani kwa muda wa saa karibu moja. Baada ya mkutano huo, alielezea furaha yake na kusema ameafikiana mambo mengi na kiongozi huyo wa Ujerumani, ambaye amempokea kwa mara ya kwanza mjini Berlin.

Emmanuel Macron, mgombea wa "En Marche!" katika uchaguzi wa urais, anaongea na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin, Machi 16, 2017.
Emmanuel Macron, mgombea wa "En Marche!" katika uchaguzi wa urais, anaongea na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin, Machi 16, 2017. REUTERS/Fabrizio Bensch
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron ameondoka katika Ofisi ya Kansela wa Ujerumani akitabasamu. Kisha akaenda kukutana waandishi wengi wa wa habari wa Ufaransa na Ujerumani ambao walikuwa wakimsubiri. Mgombea wa En Marche! amebaini kwamba mazungumzo na Angela Merkel yamefika "wakati muhimu wa kampeni. "Wakati ambapo ana matumaini ya kuibuka mshindi wakati ambapo François Fillon amepoteza uaminifu kwa sababu ya mashitaka yanayomkabili.

Nchini Ujerumani, hatari ya chama cha Front National imechukuliwa kwa umakini. Suala hili limejadiliwa wakati wa mkutano kati ya Emmanuel Macron na Kansela. Mgombea urais amesema kwamba Bi Merkel ameonyesha "nia yake ya kufanya kilio chini ya uwezo wake ili nchini Ufaransa baadhi ya vyama visiwezi kupata ushindi." Pamoja na François Fillon ambaye ana matatizo makubwa, chaguo la Macron linaonekana kuwa litachukuliwa kwa umakini nchini Ujerumani kwa kumzuia Le Pen.

Emmanuel Macron amesema kama atashinda ataimarisha ushirikiano kati ya Ufaransa na Ujerumani. Na ana imani kwamba ataibuka mshindi wa uchaguzi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.