Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU

Bunge la Uingereza latoa idhni ya kujiondoa EU

Baada ya kupitisha Jumatatu hii, Machi 13 rasimu ya sheria ya serikali ya Uingereza, Bunge la Uingereza (Westminster) limetoa rasmi mamlaka kwa Theresa May kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Makao makuu ya Bunge la Uingereza (Westminster), tangu mwaka 1547.
Makao makuu ya Bunge la Uingereza (Westminster), tangu mwaka 1547. DR
Matangazo ya kibiashara

Baada ya wiki kadhaa za mjadala ni hatua nyingine kuelekea kujitoa katika Umoja wa Ulaya EU ambayo ilifikiwa siku ya Jumatatu nchini Uingereza.

Serikali ya kihafidhina ya Theresa May hatimaye ina uwezo tosha wa kutumia Ibara ya 50 ya Mkataba wa Lisbon ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Baraza la wawakilishi na lile la Seneti havikupinga rasimu ya sheria ya serikali ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya, badala yake ziliunga mkono na rasimu hiyo inatarajiwa kuwa sheria Jumanne hii Machi 14.

Serikali ya Uingereza inapanga kuanza hatua rasmi za kujiondoa ndani ya jumuiya ya Ulaya ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Hatua hii inatarajiwa kuwa na utata kufuatia tangazo la Scotland linalodai kuwa wanampango pia wa kuwa na kura ya maoni kuhusiana na kujitenga kwao na Uingereza na kisha kuwa taifa huru.

Waziri Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 50 na uwezo kuitisha mchakato huo mapema zaidi kuanzia Jumanne hii Machi 14.

waziri Mkuu wa Uingereza anatarajiwa Jumanne hii kujieleza mbele ya Bunge kuhusu kujitoa katika Umoja wa Ulaya kinyume na jinsi vyombo vya habari vya Uingereza vinavyofikiria. Ofisi yake imeonya kuwa Theresa May hatazungumzia kuhusu Ibara ya 50 wiki hii, lakini mwishoni mwa mwezi huubaada ya kufanyika matukio muhimu mawili: Uchaguzi Mkuu Uholanzi kisha maadhimisho ya miaka 60 ya mkataba wa Roma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.